Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-17

MO Music afichua siri ya kutengana na Baraka


Nyota wa Bongo Fleva kutoka jijini Mwanza MO Music amefichua sababu ya kundi la Wazawa, na kueleza kuwa ugomvi binafsi wa T Nocks na Baraka The Price ndiyo uliopelekea kundi hilo kuvunjika.

Mo Music alikuwa ni memba wa kundi hilo lililokuwa likiundwa na wasanii kutoka lililojulikana kwa jina la WAZAWA, lililokuwa likiundwa na yeye (MO Music), Baraka The Prince pamoja na T Nocks. 

Mo aliongeza kuwa "Kila mtu ana akili zake tofauti na utofauti huo ndiyo uliopelekea Wazawa kushindwa kudumu, mara nyingine miongoni mwetu wengine walikuwa wanajiona bora zaidi ya wengine".

Pia Mo Music aligusia kwa kusema sababu ya ugomvi wa Baraka na T Nocks kuwa ni wimbo wa So Fly, wimbo ambao ulimtambulisha Baraka vizuri hasa kwa mkoa wa Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina