Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Tulia Ackson amewataka wabunge wawe na utayari wa kuisimamia na kuishauri serikali katika matumizi ya fedha zilizopitishwa katika bunge la bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo badala ya kuishia kuilalamikia serikali.
Mhe naibu spika Dk Tulia Ackson anatoa rai hiyo katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu namna ya kuandaa na kusimamia bajeti ya serikali ambapo amesema jukumu la kusimamia fedha za bajeti si la serikali peke yake kama ambayo imezoeleka kwani baada ya kumalizika kwa bunge la bajeti na bajeti kupita wabunge wengi wamekuwa akijisahau kufuatilia matumizi ya fedha hizo.Akizungumzia mafunzo hayo mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
Mhe Hawa Gahsia amesema yamekuja kwa muda muafaka huku mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa mitaji ya umma Mhe Albert Obama akiwata wabunge kushirikiana na serikali katika uhimizaji wa makusanyo ya mapato ili bajeti inayotengwa iweze kutekelezwa kama ilivyo makusudio yake.
Amina Makilagi ni mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM ambaye amewataka wabunge kuenda kukagua miradi vijijini hasa katika maeneo ya vijijini kwani huko ndiko kunaongoza kwa matumizi mabaya ya fedha badala ya kusubiri mahesabu na kukuta tayari mambo yameshaharibika.
Mafunzo hayo ya siku nne yamewakutanisha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati za bunge za hesabu za serikali za mitaa (LAAC), kamati ya hesabu za serikali (PAC) kamati ya bajeti na kamati ya uwezeshaji na uwekezaji (PIC) chini ya ufadhili wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP).
No comments:
Post a Comment