Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-22

Polisi waruhusu mikutano ya ndani ya vyama vya siasa


Jeshi la polisi nchini limeondoa marufuku ya mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kwa madai kwamba limeridhishwa na hali ya kiusalama iliyopo nchini.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani   Mssanzya ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.

Mssanzya amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba. 

"Maandamano na mikutano ya hadhara imezuiliwa hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika," amesema Mssanzya

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina