MAHAKAMA ya Mwanzo ya Masumbwe Wilayani Mbogwe imemuhukumu kifungo jera miezi 36 na kuchapwa viboko 24 matakoni Mganga wa Jadi (Sangoma ) Sabas Majaliwa (42)mfipa mkazi wa Mwanza baada ya kumtapeli mlemavu wa miguu Paul Mpangabule kwamba atamtengenezea fedha za utajiri kwa njia ya majini .
Hakimu wa mahakama hiyo ya mwanzo masumbwe mh Sunga Emmanuel Mechara amesema kifungu cha 32 cha kanuni za mwenendo wa mashauri ya jinai katika mahakama za mwanzo ambayo ni nyongeza ya tatu ya Sheria ya mahakama za mahakimu sura ya 11 iliyofanyiwa mapitio 2002.
amemuhukumu Sabas Majaliwa kwa kosa la kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 sura ya 16 kanuni ya adhabu.
Mh Mechara amesema Sabas Majaliwa ametiwa hatiani baada ya kukiri shitaka aliloshtakiwa nalo na amepewa adhabu ya kifungo jera miaka 3 sawa na mizi 36 pamoja na kuchapwa viboko 24 matakoni baada ya kupimwa na daktari ili iwe fundisho kwa waganga wengine wa jadi wanaendesha mchezo huo wa utaperi wa kuwatengenezea fedha za majini ili watajirike.
Mahakamani hapo ilidaiwa kuwa majaliwa siku ya agosti 20 mwaka huu alimtapeli sh. 435,000 Paul Mpangabule 53 mlemavu wa miguu yaani kiwete mkazi wa mtaa wa shy A nyakafuru akiwa yeye na mke wake watengenezewe fedha za utajiri za majini,ili watajirike.
Mganga huyo baada ya kuchukuwa fedha sh 435,000 alifika na vitambaa viwili cheupe na chekundu chungu kidogo ,udi na ubani na sanduku kubwa litakalojazwa fedha na chupa aliyodai inamafuta ya Binadamu ambayo yalipakwa kwenye fedha hizo wakainamishwa kwenye sanduku na kuogeshwa fedha baada ya hapo mganga akatoweka na fedha hizo akidai anazipeleka makaburini kufanya tambiko .
Aliporudi mganga akawaomba sh. Milioni tatu ili wazichanganye na fedha za majini watakatishe fedha hizo na zile za jasho lao wakakosa akawaambia wakakope ili wazilete waanze kuhesabu ndipo walipopata ufahamu na hatimaye askari polisi kituo cha masumbwe wakamkamata na kumfikisha mahakamani.
Mshitakiwa majaliwa ameomba apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mke ,watoto na mama yake mjane anaowatunza na wanamtegemea.
No comments:
Post a Comment