Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-22

TETESI za Bifu Kati ya Raymond na Harmonize Kutoka WCB, Meneja Wao Akanusha

Meneja anayewasimamia wasanii wa WCB wakiwemo Harmonize na Raymond, Ricardo Momo, amekanusha tetesi kuwa mafahali hao wamekuwa wakivimbiana na kwamba kila mmoja anajiona bora.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Ricardo amedai kuwa wawili hao wanaishi kwa upendo mkubwa.
 

“Hayo ni maneno tu, sisi tunaishi kama ni familia moja, natamani siku moja uje uone tunavyoishi, tunataniana , tupo kwenye shida tunasaidizana,” amesema.

“Hakuna hata mmoja mwenye ugomvi na mwenzake, hayo ni maneno tu ya watu wa nje, hakuna matatizo yoyote yaliyotokea kati ya Harmonize na Raymond.”

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina