Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea
Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na
Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti
uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa
jadi.Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana
baada ya kufanya uharibufu wa viti
Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali
itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.
Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya
Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile
walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi
hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
No comments:
Post a Comment