Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.
Akizungumza jana Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema alisema utekelezaji wa majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.
Alisema pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa kimedhihirika kwa vitendo alivyotendewa Lissu.
"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake"alisema Lema.
Alisema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.
No comments:
Post a Comment