Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2017-11-22

Lowassa : Sina mpango wa kurudi CCM

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa alisema jana Jumanne  kuwa  amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  .

Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina