Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2017-11-20

Mugabe Ang’olewa Uenyekiti Wa ZANU- PF.....Mkewe Avuliwa Uanachama

Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, kimemtimua Rais Robert Mugabe, kwenye uenyekiti wa chama na kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais kabla ya kufutwa kazi na Mugabe, Emerson Mnangagwa kuongoza chama hicho.

Anatakiwa ajiuzulu mwenyewe urais au kung’olewa madarakani kwa lazima kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la nchi hiyo.

Vilevile chama tawala ZANU-PF kimemfutia uanachama mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe. Hatua hiyo inamnyang’anya moja kwa moja cheo cha uenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho.

Washiriki wa karibu wa Rais Robert Mugabe katika chama alichokianzisha wamemtaka kiongozi huyo kuondoka madarakani kufuatia shinikizo kubwa la maandamano linaloendelea nchini humo sanjari na jeshi kuingilia kati.

Katika kikao hicho kinachoendelea leo, Novemba 19, viongozi wa juu wa chama hicho wanalenga kuzungumza iwapo wamuondoe kiongozi huyo kwenye chama ama la huku umoja wa vijana wa chama hicho ambao walionesha kuwa watiifu kwa kiongozi huyo na mkewe muda wote nao wakimgeuka.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina