Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-02-15

Waziri awasimamisha kazi wakurugenzi MSD





Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi leo wakurugenzi wanne wa Bohari ya Dawa (MSD) kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.5.
Mwalimu amewataja wakurugenzi hao kuwa ni Mkurugenzi wa manunuzi Heri Mchunga, Mkurugenzi wa Huduma za Kanda na Wateja Cosmas Mwaitani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Joseph Tesha, pamoja na Mkurugenzi wa ugavi Missanga Musa.
Waziri pia amesema ameshamwagiza Mkuu wa Bodi ya Bohari ya Dawa kuwaandikia barua za kusimamishwa kazi wakurugenzi hao ili uchunguzi dhidi yao uweze kuanza mara moja.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina