Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-03-26

MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AAPISHWA RASMI LEO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Miongoni mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. 

Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali. 
Viongozi mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
 

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina