Jeshi la Polisi Wilayani Bukombe Mkoani Geita limemfikisha Mahakama ya wilaya Paul Stephen (28) mkazi wa majengo mjini Ushirombo na wenzake wawili kwa wizi wa mafuta ya Dizel lita 320 zenye thamani ya sh.573,360 walizoiba machi 14 saa kumi usiku mjini Ushirombo.
Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya Veronika Seleman, mwendesha mashtaka wa Polisi Elias Mgobera alisema washtakiwa wote watatu mnamo machi 14 majira ya saa kumi usiku waliiba mafuta aina ya Diszel lita 120 zenye thamani ya Sh.195360 mali ya Mussa Sospiter wa Ushirombo huku pia ikisadikika waliiba tena mafuta aina Dizel lita 200 zenye thamani ya Sh. 368,000 ambayo mali ya Godliver Kimaro.
Washtakiwa hao wamekana shtaka kwa pamoja na hakimu veronica Selemani amewarudisha lumande hadi april 13 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika hatua nyingine kesi hiyo ilipelekea ugomvi kati ya Askari polisi na Maafisa wa TAKUKURU huku ikiwa ni kitendo cha ajabu katika jamii kwani mahusiano yao kuharibika yaweza kushindwa kuleta ufanisi kwenye utendaji wa kazi.
No comments:
Post a Comment