Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba. |
Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kutambua kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kinaweza kuthaminishwa na maisha ya mwanadamu na kwamba wananchi hawana sababu ya kuendelea kupigana na kutoana uhai kwa sababu ya ushabiki wa vyama.
Hayo ameyasema katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Mnadani katika mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita.
Amesema kuwa hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya mauaji yayohusishwa na mambo ya siasa mkoani hapa na Tunduma ambapo raia walipoteza maisha kwa sababu ya tofauti za kisiasa.
Aidha ametaka wafasi wa vyama kutambua kuwa wale wote ambao wamekuwa wakipigana ni vyema wakajua kuwa hakuna hata mmoja ambae anaingia bungeni kwani wabunge wa vyama pinzani na vyama tawala wamekuwa ni kitu kimoja pindi wanapokuwa bungeni na nje ya bunge.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa mfumo wa vyama vingi nchini haukuletwa kwa lengo la kuondoa amani ya nchi bali ni kudumisha demokrasia.
No comments:
Post a Comment