Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa
zoezi la uhakiki la kuabaini watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni
mpango wa kubaini wale wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi, zoezi hilo
litafatia zoezi lililo fanyika awali ambapo mkoa huo ulibainika kuwa na
watumishi hewa wapatao 334.
Mongella amesema pamoja na kumalizika kwa zoezi la awamu ya
kwanza la kuhakikiwa kwa watumishi hewa na kubainika watumishi wapatao 334
tumeamua kufanya upya zoezi hilo ili kuwa na idadi kamili ya watumishi
wanaolipwa fedha za serikali bila kuzifanyia kazi.
Amesema tayari taratibu zinachukuliwa ikiwa ni pamoja kuunda
jopo la kuhakiki kutoka ngazi ya mkoa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa
huo kwa ajili yakufanya uhakiki upya wakiwa na Payroll.
“Nimesha muagiza
Katibu Tawala wa Mkoa, kuwa, Wakurugenzi wote kufika kesho( leo) saa 6.00
kamili mchana yaani tarehe 05.04.2016 (Pay roll) zote ziwe zimewasilishwa
mezani kwake, ili wataalam kutoka ngazi ya mkoa waweze kwenda nazo wilayani kwa
ajili yakufanya uhakiki upya” alisema Mongella
na kuongeza:
”Tunataka kwenda
kufanya uhakiki wa mtu kwa mtu (physical), popote pale walipo warudi wahakikiwe
labda kama yupo masomoni nje ya nchi."
Ameagiza wale wote walioko masomoni, likizo au safari warudi
mara moja kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya zoezi la uhakiki, huku
akiwataka wote watakao kwenda kwa ajili ya kuhakikiwa waende wakiwa na picha
tatu za passport size, ambapo taratibu zakuweka kumbukumbu sahihi zitafanyika
“Tunataka zoezi hili
lichukue muda wa siku saba tu na baada ya hapo tutatoa ripoti kamili, tusishangae
kuona idadi hiyo ikiongezeka au kupungua kwani katika uhakiki huu naamini
tutapata majibu sahihi "alisema Mongella.
Aidha alisema hata kuwa na mzaha na yeyote atakayebainika kulea
matatizo ya watumishi hewa katika mkoa huo, hivyo lazima kila mmoja awajibike
kwa nafasi yake aliyo ajiriwa nayo.
Katika hatua nyingine Mongella, amevitaka vyombo vya habari
katika mkoa huo kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake
ya ulinzi na usalama, kusimamia maendeleo na kujua ustawi wa watu wa Mwanza
“Mwandishi wa
habari hatofautiani na kachero wa Polisi, sasa tusaidiane kuongoza huu mkoa
kwakupeana taarifa, maana mkoa huu ni mkubwa, sio rahisi kwa Mkuu wa mkoa kujua
yote yanayoendelea hadi ngazi ya kijiji lakini kwakuwa ninyi wenzangu mnao wigo
huo basi tusaidiane ili watu katika mkoa huu waweze kufanya kazi zao kwa amani
na salama."Alisema Mkuu huyo wa
Mkoa wa Mwanza.
No comments:
Post a Comment