Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-04-05

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI MKOANI GEITA

Watu wawili wafariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa huku mama mmoja ajulikanaye kwa jina la felista mganga mwenye umri wa miaka 65 avunjika miguu yote baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu.

Tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha busaka tarafa ya nyamilembe wilayani chato mkoani hapa huku eneo la tukio likiwa limefungwa na liko chini ya ulinzi ,baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameelezea jinsi hali ilivyokuwa.

Pamoja na ajali hiyo wachimbaji hao wamepaza sauti zao kwa Serikali na kuiomba iwapatie maeneo salama ya kuchimba dhahabu kama ilivyowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana.
Kaimu Afisa madini mkoa wa Geita Bw.Fabiani Mshai amesema wachimbaji hao walivamia eneo hilo baada ya kugunduliwa na mchoma mkaa mmoja, katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa Geita limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Lakini ikumbukwe kuwa mwezi uliopita tukio kama hili liliweza kutokea katika kijiji cha mgusu mkoani hapa na kupelekea watu watano kupoteza maisha huku wengine nane wakiwa wamefukiwa na kifusi.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina