Mvua na nguzo za Tanesco kuwa ndani ya barabara ya jimboni mkoani Geita ni sababu ambazo zimepelekea kuchelewa kukamilika kwa wakati ujenzi wa barabara hiyo yenye kilomita 2.2.
Mkuu wa mkoa wa geita meja jenereali mstaafu Ezekiel Kyunga ameeleza sababu hizo ofisini kwake wakati akizungumza na Storm habari kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mbunge wa jimbo la Geita vijijini mh Joseph Msukuma hivi karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato mbele ya Rais wa Tanzania dk. John Pombe Magufuli, ambapo mbunge huyo alidai kuwa mkandarasi wa kampuni ya Jasco ya jijini Mwanza anayejenga barabara hiyo ameshindwa kukamilisha kwa wakati.
Mh kyunga, amesema zipo sababu za msingi zilizochelewesha barabara hiyo ambapo baadhi ya mambo yaliyokwamisha kutokamlika kwa ujenzi wa barabara hiyo ni pamoja na mvua ambazo zinaendelea kuyesha mkoani Geita.
Katika hatua nyingine mh Kyunga amesema kuwa katika kikao cha RCC kilicho keti mwezi disemba mwaka jana chini ya mkuu wa mkoa aliyekuwepo bi. Fatuma Mwassa waliingiwa na wasiwasi juu utekelezaji wa mradi huo.
Aidha kwa upande wao wananchi wamepongeza kwa ujenzi wa barabara hiyo kuwa kiwango kinachotumika kwa kujenga ni cha uhakika huku wakimwomba mkandarasi huyo kupanua zaidi.
Barabara hiyo inayofadhiliwa na benki ya dunia, ujenzi wake ulianza mwezi julai mwaka jana na unatarajia kukamilika mwezi huu licha ya chanagmoto zilizopo katika kukamilisha mradi huo, huku barabara hiyo ikisubiriwa kwa hamu na wananchi kwani itaondoa kero na adha zilizopo.
No comments:
Post a Comment