Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-12

Wakali wa R&B Anaowakubali Soggy Doggy awataja Rama Dee, Nuruelly na Belle 9 kuwa ndio wasanii wake bora


Msanii mkongwe wa muziki na mtangazaji, Soggy Doggy amefunguka kwa kudai kuwa wasanii wake bora wa muziki wa R&B ni Rama Dee, Nuruelly pamoja na Belle 9 na wengine walio baki wanaishi kwa promo tu na sio uwezo.
Akiongea katika kipindi cha Enewz kinachoruka katika runinga ya East Africa Television, Soggy Doggy amesema kukaa kwake kwa P Funky Majani kama producer msaidizi kumemfanya awatambue wasani ambao hawana vipaji.

“Mimi nashangaa watu wanajipa sana maflag, mwanamuziki mzuri wa R&B Tanzania nakutajia tatu bora yangu, namba moja ni Rama Dee, namba mbili ni Nuruhelly na namba tatu ni Belle 9,” alisema Belle. “Lakini kuna watu wengine wanapewa mipromo, mimi nimekaa studio nimekaa studio Bongo Record kama producer msaidizi wa P Funk, kwa hiyo mimi namjua mtu akiimba kwenye key au akitoka, najua sauti ya mtu,”
Aliongeza, “Jamini kuna watu wanaimba, ukimsikiliza Rama anaimba, ukimsikiliza Nuruelly bad news, lakini huwezi kumkuta mtu anampa attention kidogo, mtu anasubiri aimbe kama Wanigeria, so hii imesababisha watu wenye vipaji vyao kufanya mambo mengine,”

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina