Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga amewaagiza wakuu wapya wa wilaya zote mkoani Geita kuhakikisha wanadhibiti suala la watu ambao wamekuwa wakiingia mkoani hapa kutoka nchi jirani kinyume na taratibu za sheria ya nchi kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama zilizopo katika wilaya wanazoziongoza.
Kyunga ameyasema hayo jana katika Hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa wilaya tano zilizopo mkoani hapa iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa
Amesema kuwa suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jitihada za kuleta maendeleo ya wananchi hivyo ni vyema wakawa makini kwa kudhibiti mipaka ya wilaya zao ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wageni wanaoingea nchini kwa njia za zisizo halali.
aidha Kyunga ameendelea kuwaagiza wakuu wa wilaya kuakikisha wanasimamia taratibu mbali mbali za kuhakikisha wanatokomeza ujambazi ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mabalozi wa nyumba kumi ambao wamekuwa wakihakikisha wanalinda maeneo wanayoyaongoza katika mitaa yao.
Hata hivyo miongoni mwa wakuu wa wilaya hao kutoka katika wilaya ya Geita na Mbongwe Herman Kapufi na Matha m Mkapusi wamesema kuwa ili kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa ni vyema wananchi wawaunge mkono ili kuhakikisha uhalifu unatokomezwa.
No comments:
Post a Comment