Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-06

Jiandaeni kwa ukame Oktoba hadi Disemba – Mamlaka ya hali ya hewa

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi na wakulima nchini Tanzania kwa ujumla kuhifadhi chakula na malisho ya mifugo kutokana na kutabiri ukame unaokuja mwishoni mwa mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Agnes Kijazi, amewataka wakulima kutumia chakula kwa uangalifu na kuhifadhi chakula walicho nacho huku akitaka wafugaji kuvuna mifugo kwa kipindi hiki ikiwa ni hali nzuri.
Pia amezishauri mamlaka husika kuanza mikakati ya kuzuia migogoro ya wafugaji na wakulima unaosababishwa na uhaba wa malisho na maji na utabiri huo kuharibu baadhi ya mito.
“Utabiri huu unaonesha pia katika baadhi ya maeneo mvua za wastani zinaweza kusaidia upatikanaji wa mazao kutegemea unyevunyevu uliopo ardhini na wakulima wasilianeni na maafisa ugani ili kupata msaada wa kitaalamu utakaowasaidia kukabiliana na upungufu wa mvua,” alisema.
Kutokana utabiri huo wa mvua za vuli unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu, inaonyesha mvua zitakuwa chini ya wastani hali itakayoashiria ukame katika maeneo mengi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina