|
Keki ya 88.9Storm fm sauti ya Geita. |
Kwa niaba ya uongozi wa 88.9 Storm fm pamoja na wafanyakazi wote napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee ,kwanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendeleo wake kwetu sote kwa kutubariki na kutupatia pumzi ambayo tunatumia bila ya gharama yoyote ,tunachukua nafasi hii kukushuru sana wewe msikilizaji ambae umeendelea kutufatilia kwa vipindi mbali mbali vinavyorushwa na kituo chako bora cha matangazo kanda ya ziwa.
Storm fm radio ni kituo cha radio kilichopo Mkoani Geita,ambacho kinasikika kanda ya ziwa na kwa njia ya website pamoja na tunein,ni kituo cha biashara kilichoanzishwa tarehe 18September 2014 leo hii kinatimiza miaka miwili Tangu kuwa hewani.
Kimeendelea kuwa Mkombozi Mkubwa kwa kuhabarisha na kuburudisha kupitia vipindi mbali mbali ambavyo vimekuwa vikifanyika kituoni hapo. shukrani za kipee zikwendee wewe msikilizaji ambae umeendelea kufatilia kituo cha 88.9Storm fm .
Ahadi ambayo menejimenti inatoa kwa wasikilizaji ni kutanua wigo mkubwa wa matangazo ili ambao wapo vijijini waweze kusikiliza kwa usahihi zaidi.
Pia Storm fm Itaendelea kutetea jamii ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa burudani kwa wateja na wapenzi wa Storm fm.
Tunakutakia usikivu mwema 88,9Storm fm Sauti ya Geita ,”Funguka jitambue anza sasa”.
|
Wasaa wa kupiga Self na Keki ukawadia. |
|
Kicheko cha Mwendo kasi hatariii. |
|
Haya Tunaanza kuimba .Happy birthday to you happy birthday dear Storm happy birthday to you. |
|
MD wa 88.9 Storm Fm Modesta Mselewa akawa na shughuli ya kuwarisha keki wafanya kazi wa Storm fm hapa akimlisha keki mtangazaji wa michezo Lucas Mwandu mzee wa madaruga. |
|
Mwandishi wa Habari na Storm fm na Mmiliki wa Maduka online akilishwa keki na MD Modesta. |
|
Mwandishi wa channel ten Mkoani Geita ,Valence Robart akilishwa keki na MD Modesta
. |
|
Ukawadia wasaa wa mambo ya maakuli hapa kiongozi wa kwanza kuongoza msafara alikuwa ni Mzee wa Kijiweni Orest Ngowi. |
|
Mkurugenzi wa vipindi Chris Lugoe akipata msosi. |
|
Wapenzi wa 88.9 Storm fm ,akiwemo Mkurugenzi wa crabu ya disere park. wakipata keki. |
|
Wasaa wa kuserebuka ukawadia . |
No comments:
Post a Comment