Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutangaza kuwa, Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF), jana kiongozi huyo aliandamana na wananchi na wananchama wa CUF hadi Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Akiwa ndani ya ofisi za chama, Prof. Lipumba alipata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa habari na alikuwa na haya yakueleza;
"Mimi ni kweli niliandika barua ya kujiuzulu, tarehe 5 Agosti mwaka jana, lakini baada ya uchaguzi wazee walikuja kuoniomba nirejee kwenye nafasi ya uenyekiti kwa sababu hali ya chama haikuwa nzuri kitaifa, alisema Prof. Lipumba
"Tarehe 8 nwezi wa 6 niliandika barua ya kutengua barua yangu ya kujiuzulu na kwa mujibu wa katiba yetu (CUF) kujiuzulu kwako kutakuwa kamili endapo mamlaka iliyokutua/kuchagua itaridhia maamuzi yako, hivyo Mkutano Mkuu haukuwa umekutana kupitisha barua yangu ya kujiuzulu hivyo nilivyoandika barua ya kutengua, nilirudi kuwa Mwenyekiti wa CUF.
"Baada ya mvutano mrefu, tuliandika barua kwenda kwa Msajili wa Vyama, akamuita Katibu Mkuu wa CUF na timu yake, akawaita na walalamikaji, na wazee pamoja na mimi ili aweze kulisuluhisha.
"Na baada ya yeye kusikiliza, ametoa msimamo wake kuhusu mgogoro wa uongozi wa CUF ambapo amesema mimi bado ni mwenyekiti halali wa CUF hadi sasa", alisema Prof. Lipumba
Katika msimamo uliotolewa na msajili wa vyama akielezea kwanini Prof. Lipumba ni mwenyekiti halali wa CUF alisema kuwa ni kwa sababu Mkutano Mkuu haujaipitisha barua yake ya kujiuzulu wala haujakataa barua yake ya kurejea kazini, lakini alichoambiwa ni kuwa asienze kazi Juni 10 kama alivyokuwa ameeleza kwenye barua yake.
Aidha, Prof. Lipumba alihitimisha kwa kusema kuwa Kamati iliyoteuliwa kuongoza chama ni batili kwa sababu hata kikao kilichowateua ni batili na hivyo kamati hiyo isijaribu kuongoza chama hicho kwani yeye ndiye mwenyekiti wa CUF.
No comments:
Post a Comment