Wananchi
waliojichukulia sheria mkononi jana wamewaua kwa kuwachoma moto watu
watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana
kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa
pikipiki.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yalifanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia jana baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa jana majira ya saa nne asubuhi.
Inaelezwa
kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili
waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki
tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.
Afisa
mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio
hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria
mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.
Miili
ya marehemu hao ilichukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na
kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya
ya Kahama
Mkuu
wa polisi wilaya ya kahama Mussa Mchenya mwenye kofia nyeusi akiwa eneo
la tukio akishuhudia eneo ambalo watuhumiwa hao wamechomewa moto.
Wananchi wakiwa katika makazi ya mtuhumiwa aliyechomwa moto wakishuhudia nyumba ikiteketea.
Shimo ambalo mtuhumiwa inadaiwa alificha pikipiki tatu ndani yake.
Wananchi wakiendelea kubomoa nyumba ya mtuhumiwa
Maafisa
wa polisi wakiwa wameifikisha miili ya watuhumiwa kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
No comments:
Post a Comment