Mchungaji
Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na
kudai anawashangaa viongozi wa kiroho wanaokaa kimya na kuacha masuala
ya uhalifu yakiendelea katika nchi bila ya kusema lolote juu ya hilo.
Mchungaji
Gwajima amesema hayo akiwa Kanisa kwake leo Jumapili ambapo aliahidi
kumfanyia ibada maalum ya kumuombea mbunge wa Singida Mashariki
(CHADEMA), Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika
akiwa nyumbani kwake Dodoma siku za hivi karibuni.
"Naona
huruma sana kwa watu wanaofanya uhalifu katika nchi kwa sababu
unapomwaga damu ya mtu na wewe yako itamwaga na mwingine bila ya
kujarisha umemwaga kwa sababu zipi. Damu imekuwa ikimwagika sana katika
nchi hii kuanzia kule Kibiti. Nashangaa sijui imekuwaje viongozi wa
kiroho walikuwa kimya, mimi sikuwepo. Viongozi wa kiroho ni lazima
waseme", amesema Gwajima.
Aidha,
Mchungaji Gwajima katika maombi yake amewataka watu wanaofanya vitendo
vya uhalifu nchini wafanye hima kutubu dhambi zao juu ya wanachokifanya
na endapo hawatafanya hivyo basi watambue yatawafika yale yale ambayo
walikuwa wakiwatendea wenzao.
"Mambo
ya kiuhalifu tunatakiwa kuyakemea bila ya kuwa na uoga wa aina yeyote
wala kuangalia upande wowote ule na hivyo ndivyo Mungu anavyotaka,
unasema unachotakiwa kusema kama hiki hakipo sawa. Tundu Lissu ana baba,
mama, watoto pamoja na mke anatakiwa kuishi", amesisitiza Gwajima.
Kwa upande mwingine, Gwajima amesema hakuna jambo baya kama kuwepo katika nchi halafu hutambui inaeleka wapi.
No comments:
Post a Comment