Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2017-09-06

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) yafanya mazungumzo yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda

Related image
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, leo  amefanya mazungumzo na Serikali ya Muungano wa Tanzani
a kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda huku yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati  ya Tanzania na FAO.


Akizungumza na Wandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Tzeba alisema kuwa ujio wa Bw. Graziano da Silva nchini unaakisi ushirikiano bora uliopo kati ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) ambapo hivi karibuni ILO walisaidia katika kuandaa mpango wa kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa fedha ya kutengeneza programu ya kutoa maarifa kwa wananchi ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo.

Aidha amesema Dkt Tzeba FAO wametoa simu 50 na Kompyuta 15 kwa wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya wataalamu wake kuwa na urahisi wa kukusanya taarifa na kuzifikisha kwa jamii.


Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali, na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed huku Ziara hiyo  ikijili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 
Na James Salvatory

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina