Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo
Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.
Akizungumza
mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea
amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na
kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34
(1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mheshimiwa
Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika leo (jana) baada ya
kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika
hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.
Mheshimiwa
Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa
Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
kwa hatua zaidi.
“Kanuni
zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia
kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa
Bungeni,” alisema.
No comments:
Post a Comment