Rais
wa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ametoa sifa na pongezi kwa rais mstaafu wa awamu ya
Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha ujenzi wa hospitali ya
Mloganzila.
Rais
ametoa pongezi hizo jana wakati akihotubia wananchi waliohudhuria
ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam.
“Wakati
ujenzi wa Hospitali hii unaanza mimi nilikuwa naagizwa tu na niliambiwa
nikatafute eneo kubwa nikawaza nitalitoa wapi lakini baadae mzee Jakaya
akanipigia tena simu akaniambia kuna eneo huko Mloganzila ni la
serikali nenda kaangalie na ujenzi uanze haraka, ndio nikaja hapa”,
alisema Rais Magufuli.
Rais
magufuli aliongeza kuwa “Watu tunapenda sifa lakini hizi sifa sio zangu
ni za rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwani
mimi nilikuwa naagizwa tu nikiwa waziri wa Ujenzi, ndio maana nimeona
niseme wazi kuwa sifa zote zimwendee mzee Kikwete”.
Aidha
rais Magufuli aliweka wazi kuwa wakati anakwenda kuona eneo la
Mloganzila wala hakukuwa na barabara lakini aliambiwa na rais Kikwete
aanze ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara haraka iwezekanvyo na
alifanya hivyo sambamba na waziri wa maji amnbaye naye aliagizwa kuanza
ujenzi wa miundombinu ya maji.
Rais
Magufuli amesisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali na Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya
Mloganzila jijini Dar es salaam ni mpango na jitihada za rais wa awamu
ya nne.
No comments:
Post a Comment