Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amesikitika kutohudhuria
kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya na kusema alipata mwaliko kuhudhuria
sherehe za kuapishwa Kenyatta lakini ameshindwa kutokana na kuingiliana
kwa majukumu.
Leo
baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya Ilidai kuwa Rais mstaafu wa
Tanzania Jakaya Kikwete ni mmoja wa wageni ambao wamehudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta jambo ambalo Jakaya Kikwete amelipinga kwa
kusema ameshindwa kwenda Kenya kutokana na majukumu kuingiliana.
Jakaya
Kikwete ametumia mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake wa
pongezi kwa Kenyatta kuchaguliwa tena kuongoza nchi ya Kenya ambayo ni
nchi rafiki na Tanzania kwa miaka mingi sasa.
"Nakupongeza
Rais UKenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi rafiki ya Kenya.
Nakushukuru kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwako.
Nasikitika sitaweza kuhudhuria kutokana na kuingiliana kwa majukumu.
Nakutakia kila la kheri katika awamu yako ijayo" alindika Kikwete
Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais kwa Kenya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017
No comments:
Post a Comment