Ikiwa leo ni siku ya kukumbuka watu wenye uaribino duniani,wananchi mkoani Geita wameiomba serikali kuhakikisha inaweka mipango madhubuti katika kutokomeza mauaji yanayohusisha watu wenye ualibinism nhini
Storm habari imezungumza na baadhi ya wananchi ambapo wamesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kuwaua kwa madai ya kupata mali jambo ambalo halina ukweli wowote na kwamba serikali inatakiwa kuweka mikakati madhubuti ili kuthibiti suala hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo storm habari imezungumza na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo,ambapo amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa likitumia mbinu mbalimbali ili kuthibiti mauaji hayo kwa kuwatumia polisi jamii ambao wapo kuanzia ngazi ya vitongoji, ikiwemo pia viongozi wa dini.
Aidha kamanda ametoa wito kwa wananchi kuachana na imani potofu zinazosababishwa watu kufanya vitendo hivyo huku akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapokuwa na mashaka na baadhi ya watu wanaodaiwa kujihusishwa na vitendo hivyo.
Siku ya albinism duniani ni siku ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 13 june lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watu wenye albinism na kutoa uelewa zaidi kwa watu hawa.
No comments:
Post a Comment