Mwanaume mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40 jina halijafahamika, ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kupigwa hadi kupoteza maisha na wananchi wenye hasira kali baada yakumkamata akifanya kitendo cha wizi wa kuku 7
Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, na kusema tukio hilo limetokea baada ya mtu aliyeibiwa kuku hao kuomba msaada kwa wananchi na wananchi kumkamata mwizi huyo na kuanza kumpiga na silaha hizo mpaka kumsababishia mauti.
Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu watatu kwaajili ya mahojiano ya tukio hilo na kuwataka watanzania kuacha kufanya vitendo vya kiharifu kwa kisingizio cha kukosa ajira za kuwaingizia kipato cha kila siku, kwani vitendo hivyo vya kiharifu vinagharimu maisha yao na kuwasababishia kifo.
Amewaasa watanzania kuacha kujichukulia sheria mkononi na watumie vyombo vya usalama katika kupambana na wahalifu.
No comments:
Post a Comment