MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kung'ara katika klabu yake, KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 ugenini dhidi ya Lommel United.
Nahodha huyo wa Tanzania, Taifa Stars jana alifunga dakika ya 46 bao la tatu katika mchezo huo wa kirafiki, baada ya Kumordzi kutangulia kufunga la kwanza dakika ya 33 na Bailey la pili dakika ya 35.
Aliyehitimisha karamu ya mabao ya KRC Genk inayojiandaa na mechi za mchujo za Europa League alikuwa ni Trossard aliyefunga bao la nne dakika ya 68.
Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa; Bizot, Walsh/Castagne dk83) Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Pozuelo/Sabak dk77), Bailey/Trossard dk45, Buffalo/Karelis dk72, Samatta/de Camargo dk72) na Kebano/Tshimanga dk77.
Wiki iliyopita Samatta alifunga mabao mawili mfululizo ndani ya siku mbili katika mechi za kirafiki pia.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC, alifunga bao moja katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Bocholt Julai 1 na akafunga tena bao moja katika ushindi wa 3-0 Julai 2 dhidi ya ESK Leopoldsburg.
Mbwana Samatta ameendeleza moto wa mabao KRC Genk baada ya ja a kufunga katika ushindi wa 4-0
|
No comments:
Post a Comment