Umoja wa madhehebu ya kikristo na kiislamu Interface Mkoani Geita, imeupongeza mgodi wa dhahabu wa GGM, kwa juhudi ambazo umekuwa ukizifanya za kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika kutokana na uwepo wa mgodi huo.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kalakana ya ufundi iliyopo eneo la magogo kata ya Bomba mbili walipokuwa wamekwenda kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa na kalakana hiyo.
Mratibu wa Interface mchungaji John Marko Ndaruka amesema kuwa wameendelea kufaidika na GGM kutokana na huduma ambazo kwa sasa zinaonekana kwani hapo awali huduma hizo zilikuwa hazifahamiki hivyo wananchi wengi walikuwa hawaoni faida ya uwepo wa mgodi huo.
Kwa upande wake, shekhe Alhad Yusufu Kabaju ambae ni mwenyekiti mwenza wa taasisi hiyo ameongeza kuwa kumekuwepo na maneno kwa jamii kuwaona kwamba hakuna jambo lolote linalofanywa na GGM, kwani sababu kuu ni kutokana na viongozi wa serikali kutokuelezwa kazi ambazo zinafanywa na mgodi katika kuleta maendeleo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa dhahabu Manase Ndoloma ameeleza kuwa thamani ya miradi inaweza kufikisha Dola milioni moja endapo kila kitu kitakuwa kimekamilika katika kalakana hiyo.
No comments:
Post a Comment