Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-10

Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.

Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara .Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu wa Rais.
 
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina