Hapa Mkuu wa wilaya akimsikiliza kijana ambae ni mlemavu wa viungo katika kijiji cha Bujula.
Mkuu Wa Wilaya Ya Geita,Herman Kapufi,Amemwagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Geita,Kuhakikisha Anamwamisha Mtendaji Wa Kijiji Cha Bujula Sekile Mhagwa Kuanzia Leo Ni Kutokana Na Kuwa Na Tuhuma Za Kutumia Fedha Kiasi Cha Sh,Million 9, Kinyume Na Matumizi Ya Fedha Hizo ,Ambapo Katika Fedha Hizo Kulikuwa Na Fedha Za Watoto Waishio Mazingira Magumu,Na zingine Za Watu Ambao Wameathirika Na VVU Na Pesa Nyingine Ya Mfuko Wa Jimbo.
Hatua Hiyo Imekuja Baada Ya Mkuu Wa Wilaya Kufanya Ziara Ya Kikazi Yenye Lengo La Kuzungumza Na Wananchi Na Kutatua Changamoto Ambazo Zimekuwa Zikiwakumba Wananchi Wa Wilaya Ya Geita.
Akiwa Katika Mkutano Na Wananchi Kata Ya Bujula,Diwani Wa Kata Hiyo Amina Kanijo,Amefikisha Malalamiko Yake Mbele Ya Mkuu Wa Wilaya Akimtuhumu Mtendaji Wa Kata Kutumia Fedha Kinyume Na Utaratibu hali ambayo imesababisha baadhi ya maendeleo ya Kata hiyo kusimama.
Kutokana Na Malalamiko Hayo Ilimlazimu Mkuu Wa Wilaya Ya Geita,Kutoa Maagizo Ya Kuhakikisha Mwalimu Ambae Ametuhumiwa Na Matumizi Ya Fedha Kukamatwa Lakini Pia Mkurugenzi kumwamisha mtendaji aliyetumia fedha kinyume na taratibu zilizowekwa . "Mtendaji kama ameshalipa fedha hafai kuendelea kubaki katika kituo hiki kuanzia jumatano mkurugenzi leta mtendaji mwingine mchapa kazi ambae anaweza kuwafanyia kazi wakazi wa bujula"alisema Kapufi.
Kapufi,Amewaagiza Watumishi Wote kuwa Na Maadili Katika Kuwatumikia Wananchi Na Kuachana Na Tabia Ya Kuwa Kero Katika Jamii Wanazoziongoza.
|
No comments:
Post a Comment