Wananchi wa kijiji cha Mwamitilwa kata ya Rubanga wilayani na mkoani hapa, wamemkataa afisa mtendaji wa kijiji hicho bw, Zagalaza Juma, mbele ya Mkuu wa wilaya ya Geita mh Herman Kapufi baada ya kushindwa kusimamia shughuli za maendeleo na badala yake kushinda akiwa amelewa hali inayowapelekea kukosa mahali pa kupeleka changamoto zao.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ambaye yuko katika ziara ya kutembelea kata zilizopo wilayani hapa kwa lengo la kubaini na kutatua changamoto zinazowakabili wamesema kuwa kiongozi huyo amekuwa akishinda amelewa na kusababisha kupotea kwa mapato kijijini hapo kutokana na kukosekana kwa mtu ambaye angeweza kukusanya mapato ya kijiji.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo mh, Enos Blashi amekiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akiunga mkono kitendo kilichofanywa na wananchi hao kwani amekwisha kuonywa na afisa utumishi wa wilaya takribani mara tatu lakini akashindwa kurekebika.
Aidha mkuu wa wilaya amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kumwondoa kiongozi huyo huku akisisitiza kuwa zoezi hilo likamilike ndani ya siku 4.
No comments:
Post a Comment