Yakikutokea kama haya lazima uwe na imani kubwa, halafu lazima ukose la kusema na zaidi sana utazidi kusema asante Mungu. Hii imetokea kwa ndugu, jamaa, marafiki wa madereva waliotekwa DR Congo baada ya kuwasili uwanja wa JKIA kutoamini wanachokiona kwa ndugu zao.
Baada ya kuwasili kwa madereva hao, ndugu, jamaa na marafiki waliibua vilio na kulia baada ya kuwaona ndugu zao waliotekekwa nchini humo huku wengine wakitoa machozi ya furaha.
Waliweza kuongea na waandishi wa habari jinsi ilivyokuwa walivyotekwa na waasi waliovaa sare za jeshi zisizofanana na walivyosafirishwa kilometa 50 porini usiku na mchana wakitembea kwa magoti na kupoteza tumaini la kupona huku baadhi wakifanikiwa kutoroka na wengine kuokolewa.
Ndugu wa madereva hao walikusanyika uwanjani hapo wakiwa na shauku ya kukutana na madereva hao ambao Septemba 14, mwaka huu, walikumbwa na kadhia ya kutekwa na kundi la wanamgambo huku magari waliyokuwa nayo yakichomwa moto na hatma yao kutojulikana.
Hata hivyo, kutokana na juhudi za serikali ya Kongo na Tanzania, madereva hao walifanikiwa kuokolewa na kupatiwa matibabu ambapo Jumatano hii waliweza kurudi nchini rasmi.
Baada ya madereva hao kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka nje kwenda kuonana na ndugu zao waliokuwa wamekusanywa pembeni, lakini walipowaona tu walishindwa kujizuia na kuwakimbilia madereva hao ambao nao waliwakimbilia huku wakilia na kutamka maneno ya kumshukuru Mungu kwa kuonana tena.
Walipo maliza mazungumzo na waandishi wa habari wakakutanishwa na familia zao na ndugu zao ambapo baadhi ya familia ziliongozana na watoto wa madereva hao, ambao katika hali ya kutia simanzi baada ya kuwaona wazazi wao, waliangua kilio kwa sauti huku wakiwaita baba zao na kuwakumbatia kwa furaha.
Madereva waliookolewa kutoka nchini Tanzania na waliowasili Jumatano hii ni Kumbuka Selemani, Hussein Mohammed, Bakari Nassoro, Issa Omary, Amdani Zarafi, Adam James, Mbwana Said, Ali Juma, Athuman Fadhil na Amis Mshana.
Waliwasili katika uwanja wa ndege wa Tanzania, wakitokea Kigali, Rwanda kwa ndege ya shirika la nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment