Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya
kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda
kukimbilia Afrika Kusini.
Akizungumza
leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza
la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda
wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.
“Kosa
hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni
kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda
wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema
Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.
Kosa
jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda
wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika
atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.
No comments:
Post a Comment