Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam
linatakiwa kubadilika katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.
Mwaka jana RC Makonda katika harakati za kutatua kero za wananchi
alipewa kero ya barabara hiyo na yeye kuikabidhi kwa kampuni ya
ukandarasi Grant Tech Company ambayo ilijitolea kuikarabati barabara
hiyo kwa kiwango cha zege.
Akiongea katika makabidhiano hayo Operation Manager wa kampuni hiyo,
Bw. Maswingo alisema anayofuraha kumkabidhi mkuu wa mkoa barabara hiyo
ya kimometa 1 ambayo inaonganisha katika ya Kurasini na Kilwa Road ikiwa
imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na aina ya magari ambayo
yanatumia barabara hiyo.
“Hii barabara aliizindua mkuu wa mkoa mwaka jana mwezi 12 na sasa
hivi tunamkabidhi ikiwa imekamilika. Barabara hii ni kiungo muhimu
katika eneo hili bila shaka itachangia kuchochote maendeleo kwa mkoa wa
Dar es salaam kwa kuwa ni barabara hii ni kiungo muhimu,” alisema
Mwaswingo.
Kwa pande wa mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alisema
barabara hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa
kuwa itawarahishia wafanyabiashara kutoa mizigo yao bandarini kwa
urahisi.
Mkuu
wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao
hapa jijini chini ya viwango ya kuwa kuanzia sasa kampuni hizo pale
zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi
na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka
mitatu.
"Wananchi
wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara,
wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama
hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita
haijapita" amesema Makonda .
Makonda
amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi
kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema
fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa wananchi wa Dar es
salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta
hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.
Makonda
amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga
Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni ndoto ya Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia
Tanzania ya viwanda inaendelea kutimia.
No comments:
Post a Comment