Viongozi
wa juu wa Chadema , Freeman Mbowe na Edward Lowassa wataongoza kampeni
za uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani kwenye kata 43.
Chama
hicho kimeunda Kamati za Kitaifa 10, zitakazoongeza nguvu, hamasa na
mikakati ya kampeni za uchaguzi wa marudio kwenye nafasi hizo kuanzia
kesho hadi siku ya uchaguzi.
Timu
hizo ambazo zitafanya kazi kwa kushirikiana na kamati zingine za hamasa
katika ngazi za kanda, mikoa, majimbo, kata na matawi katika maeneo
yenye uchaguzi huo, zitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman
Mbowe.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
wa chama hicho Tumaini Makene imeeleza kuwa Mbowe ataanza kuzindua
kampeni kesho katika Kata ya Saranga, jijini Dar es Salaam.
Makene
ametaja watakaoongoza timu hizo zilizopangwa kwa makundi A hadi G, kuwa
ni Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chama na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti Taifa
(Bara), Profesa Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa
(Zanzibar) Said Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama Dk. Vincent
Mashinji.
Amewataja
wengine watakaoongoza timu hizo kuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama
(Bara), John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar), Salum
Mwalimu.
Amesema
timu hizo zitasaidiwa kwa ukaribu na timu zingine tatu chini ya uratibu
na mikakati ya mabaraza ya chama, ikiwamo Baraza la Wanawake wa
Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na Baraza la
Wazee wa Chadema.
Timu hizo zitazunguka katika maeneo yote ya uchaguzi wa kata hizo 43, lengo ni kuwafikia wananchi wote kuelekea uchaguzi huo.
“Chadema tutaweza kuwafikia na kuzungumza na wananchi katika majimbo 37, halmashauri 36, mikoa 19 nchi nzima.
“Chama
kimedhamiria kuweka ushindani mkubwa na kushinda kata hizo 43 ambazo
chama kimeweka wagombea, tunaamini ushindi upo na ndiyo maana tunakutana
na wananchi kuwahamasisha na kuwasikiliza wanataka nini ” amesema
Makene.
No comments:
Post a Comment