Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2017-11-09

Mkuu wa wilaya ya Chato aahidi kuvitaifisha vyombo vya moto vinavyosafirisamaki wachanga

Image result for mkuu wa wilaya ya chato
Serikali wilayani Chato  mkoani Geita imeahidi kuvitaifisha vyombo vyote vya moto vitakavyokamatwa vikisafirisha samaki wachanga kutoka ziwani kwenda maeneo mengine ndani na nje ya wilaya hiyo.



Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Chato Bw Shabani Ntarambe wakati  akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake juu ya uvuvi haramu mbapo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanakagua magari na pikipiki kwa lengo la kuwabaini baadhi ya watu wanaosafirisha samaki wachanga kinyume na sheria.


Amesema hatua hiyo imekuja mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa madereva bodaboda  na magari ya abiria wanaotumia vyombo hivyo kutorosha samaki wachanga jambo ambalo halikubariki.



Nae mwenyekiti wa uhifadhi wa rasilimali za uvuvi BMU  wilayani humo Bw Bashiri Manampa  amesema  kuwa amejipanga kuanzisha msako mkali kwa kushirikiana na maofisa wa uvuvi wilayani humo kwa lengo la kuendelea kupambana na wavuvi haramu katika ziwa victoria.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina