Jeshi la
polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 14 kwa makosa mbalimbali wakiwemo
wanne kati yao kwa kujifanya maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na
usalama wa Taifa huku wakitumia nyadhifa hizo kujipatia mali kwa njia za
udanganyifu.
Kamanda wa
jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake amewataja waliokamatwa katika tukio hilo kuwa ni Shaban Ramadhan
Kwiyela (58) mkazi wa Igunga Tabora, Emmanuel Kasunga ( 45) mkazi wa Mtera
Iringa, Juma Almasi Pembambili (33) mkazi wa Sai jijini Mbeya pamoja na Emmanuel
Hassan Mwangolela (50) mkazi wa mtaa wa Ghana jijini Mbeya.
Katika tukio
la pili wamekamatwa watu wawili kwa kujihusisha na wizi wa pikipiki huku
wakitumia mbinu ya kuiba pikipiki kutoka Dodoma na kwenda kuziuza Kiteto
Manyara na zingine wakiiba kutoka Kiteto na kuzileta kuziuza hapa Mkoani Dodoma.
Kamanda
mroto amesema tukio la tatu wamemkamata kijana Abdalah Hamza Salum (20) dreva
wa bodaboda mkazi wa Area A Dodoma kwa kosa la unyang’anyi ambapo hutumia
pikipiki yake yenye namba za usajiliu MC. 366 BJR aina ya boxer kukwapua mikoba
ya wapita njia na akipakia abiria huwapeleka katika maficho na kuwatishia sime
kisha kuwapora vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi, mikufu na vito vya
thamani.
Katika tukio
la mwisho kamanda Mroto amesema wanawashikilia watu 6 akiwemo raia wa china kwa
kosa la kuchezesha mchezo wa kamali bila kibali maalumu katika mkoa wa dodoma
na hivyo kuikosesha serikali mapato na katika matukio yote kamanda mroto
amesema mkoa wa dodoma utaendelea na kila aina ya uhalifu utakaojitokeza katika
mkoa wa Dodoma
Imekufikia
ReplyDelete