Kufuatia agizo la serikali la kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi kidato cha 4, baadhi ya shule za msingi mkoani hapa ikiwemo Lutozo ,Ludete, na Nyawilimilwa zimeonekana kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi huku shule hizo zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu, madawati, na vyumba vya madarasa hali ambayo inapelekea wanafunzi kusoma wakiwa chini ya mti na wakati mwingine hulazimika kurudi nyumbani pindi mvua zinaponyesha kutokana na kukosa mahali pa kujikinga.
Wakizungumza na Storm habari walimu wakuu wa shule hizo Lukas Mabula wa Ludete, Hoza Mayunga, wa Nyawilimilwa,na Masota Elioza wa Lutozo, wamesema kuwa changamoto hizo zimekuwa zikiwafanya kushindwa kuifanya kazi yao kiufanisi na kwamba wameiomba serikali na wadau mbalimbali wa elimu kusaidia kuboresha miundo mbinu mashuleni ili kuendelea kukuza taaluma nchini.
Storm habari imefika katika shule hizo na kujionea namna wanafunzi hao wanavyokumbana na changamoto hizoikwemo kukaa chini huku wakiyoomba serikali kuboresha miundo mbinu katika shule zao ili waweze kusoma vizuri na baadae kupata wasomi wengi watakao saidia kuleta maendeleo nchini.
Hata hivyo afisa elimu wa shule za msingi wilayani Geita bw, Deusi Sefu amekiri kuwepo kwa changamoto katika shule hizo na kwamba amesema serikali imeeanza kuchukua hatua juu ya jambo hilo ambapo imetenga milioni 303 kwa ajili ya kutengeza madawati ikiwa ni pamoja na kusitisha baadhi ya miradi ya mendeleo iliyokuwa ikiendelea wilayani hapa ili kupisha uboreshaji wa miundo mbinu mashuleni.
Aidha afisa elimu Sefu amewaomba wadau na mashirika mbalimbali nchini kujitokeza kuchangia mashuleni ili kuendelea kuboresha taaluma nchini.
No comments:
Post a Comment