Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla jana alitumia dakika
kadhaa kutoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu tofauti iliyopo kati ya dawa za
kulevya aina ya bangi na pombe kali za viroba.
Alisema pombe yenye kilevi kilichothibitishwa haiwezi kuathiri
afya ya mtumiaji kama ilivyo dawa ya kulevya.
Ufafanuzi huo ulitokana na swali la Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya
maswala ya Ukimwi,Mohammed Amour aliyetaka kujua tofauti ya kitaalamu baina ya
bangi na kiroba kutokana na jinsi zinavyowatesa watumiaji.
Mbunge huyo wa Bumbwini Unguja alisema kuna kiwango kikubwa cha
kilevi kilichopo katika viroba kinachoweza kusababisha athari kwa watumiaji.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo kwenye ofisi ya wakala wa
maabara ya mkemia mkuu wa serikali, Dr. Kigwangalla alisema:"Madhara yanatofautina, ya muda mrefu na ya
muda mfupi.Utumiaji wa bangi unaathiri mfumo wa fahamu kwenye
ubongo, lakini pombe iliyopimwa kiasi cha alkoholi haiwezi kukuathiri."
Licha ya majibu hayo,Dr. Kigwangalla aliahidi kufuatilia suala
hilo katika mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo inahusika na
vipimo kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara.
"Nitafuatilia kwa
kina TFDA nione wanafanyaje, kwa nini viroba vimekuwa vikiuzwa mitaani tofauti
na viwango halisi vya alkoholi."Alisema
No comments:
Post a Comment