Mwandishi wa DW Salma Saidi |
Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma
Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam
kwa ajili ya kuangalia afya yake.
Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis
ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa
maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.
Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa
polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata
pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia
aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”
Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na
alikuwa akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema
ndege hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa
kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa
waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment