Watu watatu wamefariki dunia kwa kunyongwa na miili yao kuchomwa moto ndani ya
nyumba ya wageni iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Mauaji hayo yamegubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio
hilo kuwahusisha wapangaji wa nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.
Mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Kyela Kati, Boniface
Mtengela alisema waliouawa ni watatu kati ya watu wanne waliofika kwa pamoja
saa nne usiku jana.
Alisema watu hao walikuwa wanaume watatu na mwanamke mmoja
na waliouawa ni mwanamke na wanaume wawili.
Mtengela alisema wanaume wawili walijiandikisha kwa jina la Ali
Hassan na mwanamke la Mariam.
“Mwanamume mmoja
alipanga chumba namba 14, mwingine 105 na mwenye mke alipanga chumba namba
15.
"Waliokutwa wamekufa ni wanaume wawili wa vyumba na 14 na 105 pamoja na mwanamke huku mwanamume mwenye mke akitoroka,”alisema.
"Waliokutwa wamekufa ni wanaume wawili wa vyumba na 14 na 105 pamoja na mwanamke huku mwanamume mwenye mke akitoroka,”alisema.
Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kyela, Francis Mhagama alisema
uchunguzi wa miili ya marehemu hao umebaini kuwa waliuawa kwa kunyongwa kisha
kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya taa.
Uchunguzi katika eneo la tukio ulibaini miili yao iliungua,
lakini chumba na magodoro havikuungua. Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kyela Kati,
Timoth Luvanda alisema usiku wa tukio hilo hakusikika kelele zozote.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi hakupatikana
kuzungumzia tukio hilo wala kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba hiyo na kuhojiwa
katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela.
Mhudumu wa nyumba hiyo, Hagai Yohana alisema mgeni mmojawapo
aliondoka kabla ya saa 12 alfajiri akiwa na kidumu na mfuko wa rambo.
Alisema wageni wote waliandikisha kuwa ni wafanyabiashara na
hawakuwa na mizigo.
No comments:
Post a Comment