Abdi
Banda.
Siku
chache tu baada ya uongozi wa Simba kumsimamisha kwa kipindi cha mwezi mmoja
mlinzi Hasan Isihaka kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa
nidhamu,Kocha mkuu wa Simba Jackson Mayanja ameibuka na kumtolea uvivu mlinzi
mwingine Abdi Banda kutokana na kitendo kama hicho cha utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa Mayanja,Abdi Banda alionesha utovu wa
nidhamu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coast Union uliopigwa siku ya
jumamosi kwenye uwanja wa mkwakwani mjini Tanga,alipomsimamisha mchezaji huyo
kutoka benchi na kumwambia apige jaramba tayari kwa kuingia uwanjani kuongeza
nguvu.
Kwa sababu anazozijua mwenyewe,Banda aligomea agizo hilo
la kocha wake akidai kwanini asianze tangu mwanzo wa mchezo na badala yake anaanzia
benchi,kitendo alichokitafsiri kama kutoaminiwa na kocha wake.
Abdi Banda ni mtoto wa beki wa zamani wa Simba Hassan
Abdi Banda,anayetajwa kuwa alikuwa na nidhamu ya hali ya juu miongoni mwa
wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla.
“Mimi kama kocha wa Simba naweza kumpangia mchezaji
chochote cha kufanya kwa kuwa kazi iliyomleta kikosini ni kucheza mpira,sasa
nashangaa anakataa agizo langu?tena mbele ya watazamaji!,hivi mimi na yeye nani
yupo juu ya mwenzake?
“Nasema hivi mchezaji amesaini mkataba wa kufanya kazi ya
kucheza mpira kwenye klabu na kama hataki kutimiza wajibu wake kwangu hana
nafasi hata kidogo,mimi siwezi kumbembeleza wakati anajua wajibu wake.Amesema
Kocha Jackson Mayanja.
Mayanja
ameongeza kuwa anamshangaa Banda kumgomea maelekezo yake,wakati wachezaji
wengine wote wanayo nidhamu na wanamsikiliza kila anachowaelekeza.
Hata hivyo alipoulizwa kama adhabu gani atakayompa Banda
kutokana na kitendo hicho,Mayanja amesema kamati ya nidhamu ya Simba ndiyo
yenye jukumu la kuamua adhabu gani anayostahili kwa kile alichokifanya.
Huyo ni mchezaji wa pili kwa hivi karibuni kuripotiwa
kuonesha utovu wa nidhamu ndani ya klabu ya Simba,akitanguliwa na Hassan
Isihaka ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza kwa kipindi cha mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment