Kikosi cha Geita Gold |
Klabu ya wachimba Migodi wa Geita
inakaribia kupandishwa kucheza ligi kuu soka Tanzania bara baada subira ya muda
mrefu ya kuamua sakata la upangaji wa matokeo katika michezo miwili ya mwisho
ya ligi daraja la kwanza ambayo matokeo yake yameonekana kugubikwa na utata
mkubwa.
Geita iliibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kanembwa
JKT,huku Polisi Tabora wao wakichomoza na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya
maafande wa Jkt Oljoro,matokeo yaliyoibua hisia tofauti kutoka kwa wafuatilia
wa michezo hiyo,kiasi cha kulishtua shirikishao la soka nchini Tff ambalo nalo
likalazimika kuzuia kutangazwa kwa timu iliyopanda daraja kuingia ligi kuu
msimu ujao kutokana na utata huo.
Tarifa za
chini chini zilizotufikia zinasema kuwa kwa hali ilivyo upo
uwezekano wa asilimia 90% kwa timu ya Geita Gold kupandishwa kuingia ligi kuu.
Rais wa
Tff Jamal Malinzi alijitokeza hadharani kupitia akaunti yake ya Tweeter akisema
kuwa wameamua kuzuia kutangazwa kwa matokeo mpaka kamati ya nidhamu ikae na
kulijadili suala hilo.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kamati hiyo ya nidhamu ya shirikisho la mpira Tff,Abbas
Talimba,alipozungumza amesema kikao cha kwanza cha
kujadili sakata hilo kimefanyika jana (jumapili) lakini kimeshindwa kuibuka na
maamuzi kutokana na mmoja wa watu wanaotakiwa kuwemo kwenye kikao hicho
kutofika.
“tumeshindwa kufikia maamuzi kutokana na kukosekana kwa
kiongozi wa chama cha soka kigoma,kwahiyo kikao kitaendelea tena siku ya alhamis
na tungependa jambo hili liwe limemalizika siku hiyo” Amesema Talimba.
Hata hivyo alipoulizwa kama miongozi mwa watu wanaotajwa
kuwemo katika sakata hilo la upangaji wa matokeo wamo pia viongozi wa
Tff?,Talimba amesema hakuna kiongozi yeyote wa shirikisho aliyetajwa, isipokuwa
wale waliotajwa ni viongozi kutoka vyama vya mikoa.
No comments:
Post a Comment