Mama
wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema
kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipozikwa mwanaye ili
kwenda kumzika upya.
Mama
Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu
kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa
mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha
muigizaji huyo.
“Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“
“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” Mama Kanumba
“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” Mama Kanumba
Kwa
upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba
watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja
wake.
Muigizaji
Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na
hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven
Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.
No comments:
Post a Comment