Mwanamuziki
Diamond Platnumz amesema hukumu ya miaka miwili aliyopewa mwigizaji
Elizabeth Michael maarufu Lulu siyo adhabu bali ni mtihani ambao
unalenga kumfanya kuwa imara zaidi.
Amesema
mwigizaji huyo ambaye leo Jumatatu Mahakama Kuu imemhukumu kifungo cha
miaka miwili jela, amechaguliwa na Mungu kwa kuwa anaamini anao uwezo wa
kuhimili mikikimikiki.
Katika
mtandao wa Instagram, Diamond anayetamba na wimbo Halleluyah,
ameandika: "Mwenyezi Mungu ameamua kukupa mtihani huu wewe kwa sababu
anaamini wewe ni shujaa na imara...pia anaamini wewe ndio msichana pekee
unayeweza kuuhimili mtihani huu... hivyo usisononeke, Make him Proud.”
Mbali
na Diamond, wasanii wengine wametuma salamu za pole kwa Lulu akiwamo
Wema Sepetu, Mboni Masimba, Snura, Dj Choka, Dk Cheni na wengine wengi.
Dk
Cheni ambaye amekuwa karibu na Lulu kwa muda mrefu amesema huu ni
wakati wa kumuombea Lulu kwa kuwa hakuna anayejua kesho atapata mkasa
gani.
Katika mtandao wa Instagram aliweka picha ya Lulu na kuandika: "Tumuombee mtoto huyu kwa kuwa hakuna anayeijua kesho yake,".
No comments:
Post a Comment