Baada
ya mrembo katika tasnia ya filamu, Elizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa
miaka 2 jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa
filamu, Steven Kanumba, kuna mengi yanazungumzwa kupitia mitandao ya
kijamii.
Afande ameandika ujumbe huu…
Nakumbuka
vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda
taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya
zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya
ndege anaejiandaa kuruka….Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye
ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz
nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West uliokua maarufu
sana nyakati zile…
Lkn
wakati nikiwa back stage kabla sijapanda jukwaani huku usiku ukiwa
umetamalaki yaani ule usiku wa manani au usiku wa manane kama wengi
tulivyozoea kusema ingawa tunakosea nikashangaa nashikwa begani na mtu
aliyekua nyuma yangu ambapo kulikua na watu wengi tu😴…nilipogeuka
niangalie ninani aliyenishika bega”Hammad”nikamuona Lulu michael
aliyekua bado ni bint mdogo sana ingawa tayari alikua na umaarufu si
haba labda kwa sababu ya hayo maigizo yao ambayo baadae wakayaita filamu
au bongo movie lkn pia wkt flani Lulu alishawahi kuwa mtangazaji wa
kipindi cha watoto ktk kituo cha ItV…
nilipomuona
akaniamkia kwa bashasha namimi nikaitikia huku sura yangu nikiikunja na
kuwa ya kuogofya kisha nikaamuuliza kwa ukali kidogo ni kwanini yupo
pale ukumbini ktk muda ule ambao kwa umri wake hakupaswa kuwepo?..
lulu
hakua na majibu ya maana na papo hapo nikamtoa nje ya ukumbi na kisha
nikamtuma dereva wangu wkt ule alikua home boy wangu ephraim nguzo aka
bad card amrudishe nyumbani kwao haraka na ahakikishe mama yake
amempokea…
Bad
alifanya hivyo kiroho safi akarejea ukumbini na akanimbia kuwa
alitimiza yote niliyomuagiza ukizingatia na yeye badi tayari alikua na
familia hivyo aliujua vyema uchungu wa mwana…
lkn
miezi michache baadae nikaja kupigwa butwaa baada ya kusikia kuwa et
kale kabint lulu kumbe tayari kalikua na ukaribu usio wa kawaida na
baadhi ya hao wasanii mabazazi wa maigizo wasiokua na utu wala
aibu😢…niliumia sana moyoni nikiwa kama mzazi wa mtoto wa kike
ninaempenda sana na kutamani kumuona akitimiza ndoto zake muhimu kwenye
maisha kama kupata elimu kwa wkt muafaka…
lkn
niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa
hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule
msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar
tena palepale sinza msiba ulipokuwepo…sikutaka kuvaa joho la unafki
kama ilivyo kwa waTz wengi…
kwangu
hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi
ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa
sababu ya umaarufu wake…
leo
kanumba amepumzika au anapambana na Mola wake kwa kutofuata yale
maandiko yasemayo kuwa’TAMAA Ikichukua Mimba Huzaa Dhambi na Dhambi
Ikishakukomaa Huzaa MAUTI…
Kanumba amevuna alichopanda lkn Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso ktk maisha yake…
MUNGU ni mwema atamuafu Lulu amalize kifungo chake salama kama alivyompa kanumba haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema…
Mwisho wa siku wote wawili wabarikiwe kwa kutufundisha tuliobakia ili tuchague njia sahihi za kupita….DUNIA..GUNIA…
No comments:
Post a Comment